Exodus 20:8-10

8 aIkumbuke siku ya Sabato, uitakase. 9 bKwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote, 10 clakini siku ya saba ni Sabato kwa Bwana Mwenyezi Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike, wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
Copyright information for SwhKC